Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ameendelea kuhamasisha wananchi wa mkoa huo, hususan Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Mpiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kunenge alitoa wito huo Oktoba 19, wakati akihutubia kwenye tamasha kubwa la “Nyama Choma Festival” lililofanyika katika viwanja vya Stendi ya Mwandege, lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akizungumza katika tamasha hilo, Kunenge alisisitiza umuhimu wa wananchi wa Mkuranga kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi ili waweze kuchagua viongozi wanaowawakilisha vyema.
“Mkishiriki vizuri katika mchakato mzima wa uchaguzi huu, ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura, mtapata haki ya kumchagua kiongozi mnayemtaka, ambaye atawasaidia kuleta maendeleo katika maeneo yenu,” alisema Kunenge.
Aidha, Kunenge aliwahamasisha watu wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, ili waweze kuwaongoza wananchi wao kwa ufanisi na kuwaletea maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.