Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe. Abubakar Kunenge amesema Serikali itazingatia vigezo vya tathmini kwenye fidia ya mradi wa barabara ya Afrika Mashariki kwa iliyofanyika 2019 kwa wakazi wa Vijiji vilivyopo kata ya Mkange Wilaya ya Bagamoyo.
Kunenge ameyasema hayo Agosti 2, 2021 wakati alipokutana na Wananchi wa Vijiji vya Manda mazingara na Mkange ambapo, Wananchi hao wamekuwa wakilalamikia kutolipwa Fidia baada ya kuwepo Mchakato wa Ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki, Makurunge, Saadani Tanga.
Alieleza kuwa awali Tathimini ya Fidia kwa Wanachi hao ilifanyika mwaka 2019 na malipo yamefanyika kwa Wananchi Pangani Tanga. Jambo lilowatia hofu Wananchi hao ni kufanyika kwa Tathimini mpya ambayo fomula iliyotumika ni tofauti na ya mwaka 2019. hivyo kuwepo kwa Tathimini mbili kwenye mradi huo mmoja, na wakati huo huo Wananchi wa Vijiji Jirani wamelipwa kwa Tathimini ya awali.
Katika kutafutia ufumbuzi Malalamiko hayo Kunenge amewaleza Wanachi hao kuwa,"Mtalipwa Fidia kama walivyolipwa wenzenu wa Tanga, kwasababu ya Mazingira ya suala lenyewe kwamba Mradi ni mmoja Tathimini ilikwisha fanyika kilichofanya msilipwe kipindi hicho ni kukosekana kwa fedha".
"Nimelichukua tutaenda kushauriana na Wizara fidia zilipwe kupitia vigezo walivyotumia kulipa wananchi wa Vijijini Jirani na kama inavyonekana kwenye Tathimini ya awali. Tutatumia hekima pia kutafutia ufumbuzi suala hilo alieleza Kunenge."vuteni subira suala hili tunalishughulikia"alisisitiza RC Kunenge
Aidha aliwaondoa hofu Wananchi hao ambao walikuwa wanalalamikia kupunguzwa kwa fidia zao walizofanyiwa uthamini awali na baadae kuletewa taarifa ya fidia mpya wakidai kuwa imepunguzwa kutokana na mita zitakazoshushwa na wakala wa Barabara (TANROAD).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.