Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewataka Madiwani wa Halmshauri za Chalinze na Bagamoyo kujifunza masuala ya Uchumi, Ubunifu, uvumbuzi, Biashara na Masoko Ili kuzisaidia Halmshauri zao kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ya ndani na kuongeza tija katika utoaji huduma kwa jamii.
Mhe. Kunenge alisema hayo Juni 15, 2022 wakati alipohutubia vikao vya Mabaraza ya Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo kwa nyakati tofauti yaliyokuwa maalum kujadili Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali vikao vilivyofanyika katika kumbi za Halmshauri hizo.
Akiwa Chalinze, Mhe. Kunenge alibainisha kuwa vyanzo vikuu vinavyoendelea kutegemewa na halmashauri hiyo ni ya sekta ya ujenzi akitaja Kokoto na Mchanga ambavyo alisema kuwa kwa sasa vimeshuka uhitaji, pia akataja chanzo cha uuzwaji viwanja kuwa sio endelevu.
"Mapato ya Halmashauri ya Chalinze yanashuka, tuanze kuweka Mazingira mazuri na tuwe na Mikakati ya kuanzisha Vyanzo vipya, tutenge asilimia flani kwenye bajeti yetu itumike kuanzisha vyanzo vipya." Alisema Kunenge.
Katika vikao hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani aliwaelekeza wataalam wa halmashauri hizo kutumia takwimu rasmi za kiserikali kubaini fursa, kupanga nakutekeleza uanzishwaji vyanzo vipya na kuongeza mapato.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.