Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakar kunenge amewaelekeza Wakuu wa Wilaya mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Lishe ili kufanikisha azma ya kujenga afya ya Mama na mtoto katika jamii.
Aliyasema hayo leo Februari 6, 2023 wakati akifungua kikao cha taarifa ya utekelezaji Mkataba wa Lishe kimkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Ofisini kwake.
Pamoja na maelekezo hayo, Kunenge alipongeza jitihada za watekelezaji wa mkataba wa lishe mkoani humo kwa kuwezesha mkoa huo kuwa wa sita kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa mwaka wa 2021/2022.
"Niwapongeze wote, mmefanya kazi kubwa, pamoja na mkoa wetu kuwa wa 26, Halmashauri zetu nazo zimefanya vizuri kitaifa kwani Bagamoyo imekuwa ya 9, Kibaha Mji ya 10 na Kibaha DC ya 11kati ya zote 184, sasa tuongeze nguvu tupande nafasi za juu zaidi na inawezekana," alisema.
Alieleza kuwa moja ya njia za kuboresha lishe ni kupanda miti ya matunda na kuitunza huku akiwataka viongozi wa dini kutoa elimu ya lishe kwa jamii wakati wa ibada.
Kwa upande wake Ofisa lishe Mkoa huo Pamela Meena alieleza kuwa tatizo wanalokabiliana nalo ni fedha kuwa zinatumwa kwenye mfumo kwa kuchelewa, mifumo kutofanya kazi ipasavyo na Hali ya udumavu kimkoa hadi 2022 ni asilimia 23.3.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.