Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema Serikali ya Mkoa huo haiko tayari kuingilia maamuzi yaliyotolewa na Mahakama kwenye mambo mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi.
Kunenge ameyasema hayo Mei 31 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Tondoroni kata ya Kiluvya Halmashauri ya Kisarawe aliokutana nao kwa kikao cha muda mfupi Mjini Kisarawe.
Wananchi hao kwa muda mrefu wanakabiliana na mgogoro wa ardhi kati yao na kikosi cha Jeshi 83 REGT
"Msimamo wetu ngazi ya Mkoa hatuingilii maamuzi ya Mahakama kama wameshafanya maamuzi mnatakiwa kuondoka kwenye eneo hilo msije mkapata madhara vinginevyo rudini mahakamani tena," amesema Kunenge.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema wananchi hao wanatakiwa kuheshimu maamuzi ya Mahakama na endapo hawajaridhika ni vema wakarudi Mahakamani kukata Rufaa.
Hata hivyo wananchi hao walimuomba Mkuu wa Mkoa kupokea nyaraka za Mahakama walizonazo jambo ambalo alikubaliana nalo na kuwataka kuchagua wawakilishi kwa ajili ya kukutana nao June 3 siku ya jumatatu kujadiliana kuhusiana na jambo hilo.
Awali Mwanasheria wa Mkoa wa Pwani Moza Mtete aliwasilisha sehemu ya hukumu ya kesi hiyo namba 83 ya mwaka 2016 kuwa madai ya hoja za walalamikaji hoja zilizopelekwa zipo nje ya ukomo.
Moza amesema mwaka 1980 Jeshi lilitambua mipaka yake na waliokuwepo kwenye eneo la Tondoroni walilipwa fidia na malalamiko ya wananchi hao walikuwa wanadai Jeshi halijafuata Sheria ya fidia hoja ambayo ilionekana haina Msingi.
Kwa mujibu Moza sehemu ya hukumu hiyo pia ilibainisha kwamba Ili ulipwe fidia madai yanatakiwa kupelekwa ndani ya miaka mitatu tofauti na wananchi hao ambao wamepeleka madai yao baada ya miaka kumi kupitia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.