• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

RC Kunenge awataka Wananchi wa Chemchem Kutoa Ushirikiano kwa Wawekezaji

Posted on: December 30th, 2022

Serikali Mkoani Pwani, imewaasa wananchi wa kata ya Chemchem ,Utete wilayani Rufiji Mkoani Pwani kutoa ushirikiano kwa mwekezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji Sukari Lake Agro sugar estates, unaotarajia kutoa ajira zaidi ya 3,500 na kugharimu dollar za kimarekani milioni 321 ifikapo 2025.

Akitembelea na kukagua eneo la mradi huo leo Desemba 30,2022 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe Abubakari Kunenge alieleza, kwa upande wa Serikali imembariki mwekezaji huyo kuendelea na mchakato ya uwekezaji kwa manufaa chanya ya kata , wilaya, mkoa na Taifa kijumla.

Alieleza, kiwanda hicho kinakwenda kutatua uhaba wa sukari na kuondokana na uingizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.

Kunenge alieleza, kwasasa mahitaji ya sukari Nchini (brown sugar) ni tani 440,000 na sukari nyeupe ya Viwandani tani 220,000 , hivyo uwekezaji huo ni mkombozi kwa wanaRufiji.

"WanaRufiji tunafungua mkoa na wilaya hii wapo wenzenu wanalilia wawekezaji kama hawa ni wajibu wetu kuhakikisha tunatoa ushirikiano, Panapokuwa na misuguano hakuna maendeleo, elimu izidi kutolewa jamii ielewe umuhimu wa mradi huu badala ya kuweka vikwazo"

"Huwezi kupata tija kwa kuvutana, mivutano haina manufaa, kwani mradi unahitaji wananchi na wananchi wanahitaji mradi, unapochelewa mradi mnaongeza gharama za mradi kwa mwekezaji na kumpa hasara"alifafanua Kunenge.

Hata hivyo Kunenge alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa matokeo makubwa ya kazi yake inayoonekana kufanyika katika mkoa huo ikiwemo katika uwekezaji, miradi mikubwa ya kimkakati, maji,umeme, miundombinu,elimu na afya

Aidha Kunenge alieleza ni wajibu wa wazazi na walezi Rufiji Mkoani Pwani kuandaa vijana wao ili waje kunufaika na mradi huu.

"Nimetembelea viwanda 28 kila nilipopita wawekezaji wanatoa changamoto ya vijana wazawa kushindwa kuendelea na kazi ,suala ambalo linasikitisha "alibainisha Kunenge.

Naye Meneja mradi Lake Agro, Abubakar Nassoro alieleza ,wameanza Septemba mwaka 2021, ambapo wapo kwenye hatua ya maandalizi ya vitalu miche ya miwa, wamechimba bwawa la maji linalobeba ujazo wa Lita milioni 4.8,umeme na kuboresha miundombinu mbalimbali.

Alieleza, kiwanda cha sukari kinatarajia kuanza mwaka 2025 kwa kuzalisha tani 300,000 za sukari na pia watatumia kilimo cha mkataba kwa wakulima wa nje.

Nassoro alieleza ,eneo la uwekezaji ni hekta 15,000 ambalo awamu ya kwanza wamefanya tathmini na kulipa fidia kwa Wananchi 42 kiasi cha sh.milioni 172 huku awamu ya pili wanatarajia kuwalipa fidia wananchi 130 na Sasa wapo katika hatua ya kusubiri muongozo wa Serikali.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.