Madaktari Bingwa wa mama Samia 45 wamepiga kambi Mkoani Pwani ,kwa siku tano kuanzia Juni 3-Juni 7 mwaka 2024 ili kutoa huduma za afya kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo ya njia ya uzazi na watoto.
Aidha utoaji wa dawa za usingizi upasuaji wa kibobezi, magonjwa ya kawaida na kutoa rufaa kwa wale watakaohitajika.
Akizungumza Leo Juni 3 ,2024 na madaktari bingwa hao katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa Mkoa, Mkuu wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakar Kunenge alieleza udaktari ni kazi ya wito na kujitolea kuokoa maisha ya watu .
Aliwataka madaktari hao kutoa huduma bora kwani wameaminiwa na ni kazi iliyobeba maisha ya watu.
Kunenge alitoa rai,kwa wataalam wa afya na madaktari kwenda na mabadiliko ya kidunia kwa kuwa wabunifu na watafiti ili kupanua uelewa na kutoa huduma bora na Kwa utaalamu zaidi.
Alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya,kuongeza vifaa tiba ,madawa na miundombinu ili kutoa huduma bora kwa watanzania .
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani (RMO)Dkt.Benedicto Ngaiza alisema,wamejipanga na walianza maandalizi ya ujio huo tangu wiki iliyopita.
"Hamasa ni kubwa, tunatarajia wananchi wengi watajitokeza kupatiwa huduma na kupata tiba stahiki"
Ofisa mradi kutoka wizara ya afya, John Meena alifafanua, kampeni hiyo ya madaktari wa Samia kutoa huduma kwa wananchi ni zoezi Endelevu.
Mkoa wa Pwani una wilaya saba, Halmashauri Tisa, ina jumla ya Hospital 13 kati ya hizo Rufaa ya Mkoa Tumbi, vituo vya afya 50, kliniki za kutoa Huduma za kujifungulia 22 na zahanati 388.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.