Mkuu wa Mkoa Pwani mhe Abubakar Kunenge ,imeiagiza halmashauri ya Mji wa Kibaha na halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,kuhakikisha zinafunga hoja zote ambazo hazijafungwa katika ukaguzi wa hesabu za Serikali ,kwa mwaka 2019/2020 ,ifikapo September 30 mwaka huu.
Akitoa maagizo hayo Juni 17,wakati wa baraza la madiwani kupitia na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG )mwaka 2019/2020, alisema ,hoja hizo zifungwe na kama watakwama watoe taarifa.
Alibainisha hoja zinazohusisha taasisi nyingine nazo zishughulikiwe na kuhakikisha hazijirudii kwa mwaka mwingine .
Pamoja na hayo,alieleza ni wakati wa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi ambao watabainika kusababisha hasara kwa halmashauri.
Kunenge aliongeza ,adhabu itakayotolewa ilingane na ukubwa wa hasara aliyosababisha mtumishi lengwa ili kusaidia kulinda maadili na uwajibikaji.
Pia mkuu huyo wa mkoa, alielekeza ,kutenga fedha kwa ajili ya miradi iliyokwama muda mrefu .
"Epukeni kuzalisha hoja ,ongezeni wigo wa ukusanyaji mapato na halmashauri ibueni vyanzo vipya vya mapato ili kuinua mapato ." alisema Kunenge
Kunenge aliongeza ili kutekeleza ilani ya CCM ,madiwani waendelee kusimamia miradi kwa maslahi ya wananchi kwa lengo la kutunza matarajio ya wananchi.
Nae mkaguzi mkuu wa hesabu ,Mkoani Pwani Mary Dibogo ,alisema wao wapo kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwa maslahi ya jamii na serikali hivyo CAG haiwezi kuonea halmashauri yoyote .
Alitaka fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi zifanyiwe kazi husika na ijengwe kwa thamani inayolingana na fedha iliyotolewa bila miradi hiyo kukaa kwa muda mrefu pasipo kukamilishwa.
Alizitaka halmashauri hizo,kusimamia ukusanyaji wa mapato ,na kuhakikisha yanafika sehemu sahihi .
Kwa upande wake ,Katibu tawala Mkoani Pwani ,Mwanasha Tumbo alitoa rai kwa watumishi na watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea .
Mwanasha aliwaasa kufuata sheria ,kanuni na muongozo katika masuala ya ukaguzi ili kuondokana na dosari ndogondogo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.