Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameagiza kuundwa kwa Bodi ya Mpito ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Pwani CORECU kufatia kuzuka kwa Mgogora na baadhi ya wanachama hicho na kupelekea kutaka kujitoa.
Amefikia Uamuzi huo Aprili, 20,2021 Wakati wa Mkutano Maalumu wa Chama Kikuu Cha Ushirika Pwani CORECU uliofanyika Katika Ukumbi wa Kibiti Sekondari Wilayani Kibiti.
Ndikilo alieleza kuwa Chama hicho Kikuu CORECU kinalalamikiwa kwa kuchelewa kuanza Minada ya mazao ya Korosho kwa wakati, kuchelewa kusambaza Vifungashio Magunia, kuhusika katika kushuka kwa bei ya mazao, Uwepo wa Deni Sugu kwenye Mabenki linalolipwa na Vyama vya Msingi, kukosekana kwa Mahusiano mazuri katika Chama Kikuu na Vyama vya Msingi. Ameeleza kuwa sababu hizo zimepelekea vyama 28 vya Msingi kutoka Wilaya ya Kibiti na Rufiji kuwasilisha barua ya kutaka kujitoa kwenye Umoja huo,
Aidha amewambia wanachama hao kuwa kutaka kujitoa na kuunda Chama kipya ni Hiari yao, isipokuwa amewataka kujua faida na hasara endapo wataamua kujitoa katika chama hicho.
“Kama nataka kujitoa katika chama hiki cha CORECU mtapaswa kujihoji maswali Yafuatayo ikiwa pamoja na kujua Muda utakaotumika katika Mchakato wa Kuunda Chama kipya cha Ushirika Rufiji na Kibiti (Je Chama kitakuwa tayari kabla kuanza Msimu wa Ufuta na Korosho Mwaka huu 2021? Na kama hakitakuwa tayari ni chama Gani kitasimamia mauzo ya mazao hayo”.Alisema Ndikilo
Aliongezea kusema kuwa Suala hili ni la Usalama wa Wakulima na Wananchi Wengi wa Mkoa wetu hivyo linapaswa kuangaliwa kwa makini.
Amemuelekeza Katibu Tawala Mkoa kusimamia kuundwa kwa Bodi hiyo ya Mpito. Ameelekeza wajumbe hao kupendekeza majina matatu kutoka kila Wilaya ili wafanyiwe upekuzi na Vyombo vya dola kama Wana sifa ya kuwepo kwenye Bodi hiyo itakayoongoza kwa Mwaka Mmoja.
Ameitaka Bodi hiyo kwenda kufanya kazi na kuja na Majawabu ya Maswali na Changamoto za Wanachama hao ili kuwe na utulivu. Ameitaka kwenda kufuatilia Changamoto na kero za CORECU na kuja na Mapendekezo.
Ndikilo Ameeleza kuwa wamealikwa kama Viongozi na Watendaji wa Serikali kwenye Mkutano huo ili kusiliza na kushauri kuhusu Agenda ya Vyama vya Msingi Wilayani Kibiti na Rufiji kutaka kujitoa katika Chama Kikuu cha Ushirika CORECU,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.