MKuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Patrick Kenani Sawala huku akimuelekeza kushughulikia changamoto mbalimbali za wananchi ikiwa ni pamoja na migogoro ya wakulima na Wafugaji katika Wilaya hiyo.
Mara baada ya kumuapisha Mkuu huyo wa Wilaya, Mhandisi Ndikilo alimuelekeza kuhakikisha anasimamia kilimo cha zao la Korosho na ufuta ambayo yamekuwa mazao makuu ya biashara kwa Mkoa wa Pwani.
Ndikilo alisema, Wilaya hiyo ina Mambo mengi ya kufanya na mkuu huyo wa Wilaya anatakiwa kuzingatia zaidi ulinzi na usalama kwani kama hakuna amani hakuna miradi ya maendeleo itakayotekelezeka.
"Weka utaratibu na kamati ya ulinzi na Usalama kwenye Wilaya yako ili wasiwepo watu wanaoondoa utulivu uliopo na kusababisha kuvuruga amani" alisema.
Aidha alimtaka kuhakikisha hakuna jambo ambalo halimhusu na kwamba ahakikishe kila kitu anakishughulikia kwakua yeye ndio mwakilishi wa Rais katika Wilaya hiyo.
Akiongea baada ya kuapishwa mkuu huyo wa Wilaya Luteni Kanali Patrick Sawala alimshukuru Rais kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo.
Alisema, baada ya kuapishwa ataanza kushughulikia kero ambazo zimeelezwa kwa Rais ikiwa ni pamoja na kushuguulikia migogoro na kuhakikisha kila mmoja anatekeleza majukumu yake akiwa na amani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.