Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa miezi mitatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama na Ofisa Utumishi , kuhakikisha kuwa kitengo cha ukaguzi wa ndani kinajitosheleza kwa ikama ya watumishi na vitendea kazi.
Ameeleza kuwa kitengo hicho kiangaliwe kwa jicho la tatu, ili kiweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu wakati wa Ukaguzih
Akizungumza katika baraza maalum la Madiwani kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) Mhandisi Ndikilo alieleza kuwa “haiwezekani kitengo muhimu kama hiki kinachosaidia baraza la madiwani katika kusimamia fedha za Serikali kinakosa watumishi wa kutosha na vitendea kazi”.
Pia alisema kuwa kumekuwepo na changamoto za kiutendaji katika raslimali watu na fedha na kusimamia miradi ya maendeleo":Hivyo amewataka watumishi waote wa halmashauri za mkoa Pwani kuhakikisha kuwa wanaufata sheria na taratibu katika utendaji wao wa kazi ili kuweza kuondoa dosari zinazojitokeza wakati wa ukaguzi.
Katika hatua nyingine Mhandisi Ndikilo ameongezea kwamba, CAG asionekane ni adui kwani ni mshirika wa kuweka mambo vizuri kuhakikisha fedha za serikali haziliwi wala kufujwa.
Nae Mkaguzi wa hesabu wa nje mkoani Pwani, Hamis Juma ameipongeza halmashauri ya Wilaya yaKisarawe kwa kupata hati safi tena na alitaka ushauri na maoni yaliyotolewa katika hoja 26 zinazoendelea kufanyiwa kazi na halmashauri hiyo zifanyiwe kazi .
Awali akimkaribisha Mkuu huyo wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alisema halmashauri hiyo imepokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2017/2018 kutoka kwa mdhibiti wa hesabu za serikali mwezi april 2019 ikionyesha hati safi na hoja za ukaguzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.