Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo amempongeza Rais Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuazisha Tume ya kupambana na Madawa ya kulevya, pia kuwezesha kuanzishwa Kliniki ya tiba ya waraibu Wilayani Bagamoyo, aidha amempogeza kwa mpango wa kuanzisha kliniki nyingine ya waraibu katika Hospitali ya Mkoa ya Tumbi.
Pongezi hizo amezitoa 12 Agosti, 2020 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendelo na kusikiliza kero za wananchi Wilayani Bagamoyo ambapo alitembelea na kukagua ukarabati wa jengo la kliniki hiyo iliyopo hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.
Akizungumza na Waraibu hao Ndikilo alisema kuwa Serikali imefanya jambo jema sana kwa kuanzisha Kliniki hii ambayo kwa kiasi kikubwa imeweza kuwasaidia Vijana ambao walijiingiza katika matumizi ya madawa hayo. akiwapongeza waraibu hao kuachana na madawa ya kulevya alisema“Madawa ya kulevya sasa basi, Madawa ya kulevya ni hatari, yanaangamiza utu wa binadamu, yanaua nguvu kazi ya nchi Hongereni kwa uamuzi mliochuku" alisema Ndikilo.
Aliendelea kusema kuwa Rais Wetu Mhe Dkt John pombe magufuli tangu aingiee madarakani ameendelea kupambana na madawa ya kulevya na kuunda Tume ya kuthibiti madawa ya kulevya Nchini."Juhudi zetu zimefanikiwa kupambana na madawa haya, nipongeze jeshi la polisi kwa kupambana na hili, lakini bado ongezeni nguvu. taarifa anazopata za kuripoti uwepo madawa ya kulevya Mkoani Pwani zimepungua”alifafanua Ndikilo.
Aliendelea kusema kuwa , waingizaji wa madawa haya hawana nafasi kwa kipindi hiki na amewataka wananchi wazidi kuto ushirikiano katika kutokomeza biashara hii kwa kuwataja majina ya wahusika wote ili vyombo vya Dola viwashughulikie
Mkuu wa Mkoa huyo amewashauri waraibu hao kutengeneza vikundi vya ujasiriliamali ambavyo vitaweza kuwasaidia katika kuinua uchumi wao katika kuwahamasisha kujishughulisha kiuchumi aliendesha harambee ndogo ambayo ilikusanya shilingi laki Tatu na akahadi kukipatia kikundi hicho shulingi laki Tano pia Mkuu wa wilaya ya Rufiji aliahidi laki mbili na kupelekea fedha hizo ni shilingi milioni Moja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.