Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikiloametoa siku mbili kwa Viongozi wa wauza mitumba maarufu kama warumba, kupeleka orodha ya wafanyabiashara wanaofanya shughuli hiyo kwenye maeneo ya Janga na Mtongani Mlandizi Wilayani Kibaha.
Uamuzi huo umetolewa wakati Mkuu wa Mkoa wa Pwani akizungumza na Wafanya biashara wa kitongoji cha Mtongani waliogoma kufaanya biashara kwenye eneo la soko jipya kwa zaid ya wiki tatu wakidai eneo walilopelekwa kuwa ni dogo na si rafiki, huku Halmashauri ikisema sehemu wanayofanyia biashara si sahihi kwani kuna miundombinu ya umeme yaani Gridi ya Taifa na limepitiwa na Bomba la Gas.
“Nimekuja hapa kukutana nanyi ili kupata muafaka kwani hata idadi ya wafanyabiashara wangapi mpo eneo hili haieleweki , kwani Halmashauri inasema mpo 250 hadi 280 huku nyie mkisema mpo 1,000 ,hali ambayo hata ukusanyaji wa mapato yanakuwa hayana uhalisia kwani Halmashauri inasema inakusanya 100,000,kuna tatizo hapa kwa Halmashauri na wafanyabiashara” alisema Mhamdisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo ameagiza kuchunguzwa kwa suala hili lenye taarifa zinazokizana na majibu yatolewe jumatano baada ya vyombo husika kufanya uchunguzi.
“Nimetembelea maeneo yote mnayofanyia biashara hivi na kule mnakotaka kupelekwa, leo nataka miletee orodha ya wafanyabiashara wanaofanya kwenye mnada wa jumapili ili tukitoa maamuzi yawe sahihi kila upande upate haki yake”alisema Mhandisi Ndikilo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa amewaomba wafanya biashara hao kuwa watulivu na kutoa ushirikiano katika kupata ukweli wa jambo hilo ili waweze kujua hatma yao.
Mbuge Jumaa amewafafanulia wafanyabiashara hao kuwa Mkuu wa Mkoa kutaka orodha yao ni kutaka kujiridhisha na kujua ukweli wa idadi kamili ya wafanyabiashara waliopo kwani kama wako zaid ya 1,000 na fedha zinzopatikana kwenye makusanyo haya sas hakuna usahihi hivyo lazima ajiridhishe na kutoa maamuzi sahihi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.