Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka Wanachi Mkoani wa Pwani kupanda Miti kwa wingi nakuacha kukata miti ovyo ili kutunza Misitu ya asili.
Rai hiyo ameitoa leo Aprili 16, 2021 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti Kimkoa yaliyofanyika Kijiji Cha Mlingotini Wilayani Bagamoyo.
Akizungumza na Wananchi na Wadau waoshiriki kwenye Maadhimisho hayo Ndikilo ameeleza kuwa Lengo la Mkoa Ni kupanda miti 13,500,000, Amesema kuwa Kwenye msimu huu 2020/21 jumla ya Miche 6,552,254 sawa na asilimia 48.5 itapandwa kwenye Halmashauri zote za Mkoa huo, Ameeleza kuwa kila Halmashauri imepewa Lengo la kupanda Miti 1,500,000 kwa mwaka.
Akieleza umuhimu wa hafla hiyo kufanyika katika kupanda Mikoko 10,000 Kwenye eneo la Mlingotini amesema, wanapanda kuzuia Mawimbi makali, kuwa sehemu ya mazalia ya Samaki, kuzuia Mmonyoko wa udongo, kupata Nguzo na mbao, Ameeleza ataendelea kufuatilia na kuchukua hatua kwa wote wanaoharibu misitu ya mikoko,
Akifafanua kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni panda Miti kwa Uhifadhi wa Mazingira, kwa maendeleo ya Viwanda na kuimarisha Uchumi, Ndikilo amesema
"Wanadamu na Miti tunategemeana, inatupasa kupanda miti bila kujali kuwa nani atakaa au kutumia kivuli na Rasilmali ya Miti hiyo"
Amewataka Wanachi kutumia Nisahati mbadala katika Kupikia ili kupunguza matumizi ya Mkaa na kutunza Mazingira. Amewaeleza kuwa Mkoa huo una kiwanda cha kuzalisha Mitungi ya gesi, hivyo gesi hiyo inapatikana kwa urahisi.
Amezielekeza Taasisi zote za Umma na Binafsi kupanda Miti kwenye maeneo yao, ametaja kutofurahishwa na kitendo cha Ujenzi wa Shule na Vituo vya Afya mpka vinakamilia Bila ya kupanda Mti hata Mmoja. Amesema Kama Taasisi za Umma na Binafsi zitafanya hivo Mkoa utaweza kufikia lengo Upandaji Miti 1,500,000. Ameitaka Sekretarieti ya Mkoa kufanya ufuatiliaji wa Maelekezo yake na kukagua Miti itakayopandwa kuhakikisha inatunzwa hadi kukomaa.
Amepongeza Wakala wa Huduma za Misitu TFS kwa kuzalisha miche mingi 570,000 Ambayo itapandwa kwenye Mkoa wetu. Amewataka TFS kuendelea kufanya Doria ili kulinda Misitu yetu, amewasistiza Wananchi kupitia BMU kutoa ushirikiano katika kulinda Misitu hiyo.
Amewaonya Wenyeviti wa Vijiji kuacha tabia ya kufanya misitu kuwa sehemu yao ya kujipatia kipato kwa kuuza na kuruhusu uvamizi wa mifugo, Mkazi na Uchimbaji wa Mchanga, kwenye maeneo ya misitu. Ametoa Maelekezo kwa Wanachi wote waliovamia Msitu wa Ruvu Kaskazini kuondoka mara moja kabala ya Operesheni ya kuwaondoa haijaanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.