Wakulima wa matunda Mkoani Pwani wametakiwa kulima kisasa zao la matunda ya aina mbalimbali kwani soko la uhakika la mazao hayo lipo la kutosha.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist W. Ndikillo wakati alipofanya ziara yake katika kiwanda cha kuchakata na kusindika matunda cha Elven Agri Company Ltd kilichopo Mapinga Wilayani Bagamoyo na kiwanda cha kusindika juice cha Sayona kilichopo Mboga Wilayani Bagamoyo.
Aidha Mhe. Ndikilo alieleza kwamba wakulima wengi wanahitaji kulima kwa tija badala ya kupata hasara kwa kukosa masoko, pia alisema kwa kutambua hilo kuna kila sababu ya kubadilika kwa kuona umuhimu wa kulima matunda yenye ubora na yanayojiuza.
“Watalaam wa kilimo wa Mkoa ,watendaji wa Halmashauri katika Idara hii, mtoke maofisini muende kuwapa elimu wakulima hawa ili waweze kujifunza kulima kisasa ili kuwawezesha kutoa bidhaa ambazo zitawapatia soko na waweze kunufaika kwa jasho lao”. Alisema Mhe. Ndikilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.