Mkuu wa wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka watumishi wa halmashauri za mkoani hapa kuwa na ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kiserikali ili kuondoa changamoto zilizopo.
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo Mjini Kibaha wakati wa mjadala ulihohusu hali ya elimu katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mwanzoni mwa wiki.
Alisema kuwa zipo Changamoto katika Sekta ya Elimu ambazo zinahitaji ushirikiano wa watumishi wa sekta hiyo na wa sekta zingine ikiwa ni pamoja na wadau mbalimbali ili kukabiliana nazo na akaserma kuwa kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake kwa ufanisi katika sekta anayotumikia.
Mhandisi Ndikilo alipongeza uongozi wa Wilaya ya Kisarawe kwa kampeni ya tokomeza ziro na wa Wilaya ya Kibaha kwa kampeni ya elimisha Kibaha zinazoendelea katika Wilaya hizo kuwa ziimeleta mabadiliko makubwa katika kuboresha elimu kwa shule za msingi na Sekonadari.
Alisema kuwa kampeni ya elimisha Kibaha ambayo imeanzishwa na mkuu wa Wilaya hiyo mhe. Assumpter Mshama imekuwa Mkombozi kupunguza uhaba wa vyumba vya Madarasa.
“Kampeni za Elimu zinasaidia kuondoa changamoto za Elimu, nimpongeze mama Mshama hadi sasa vyumba 40 vinajengwa kutokana na kampeni aliyoanzisha na kisarawe napo kuna wale watoto wanaoshindwa kuanza kidato cha kwanza sasa changamoto hizo zitamalizwa taratibu “ alisema Mhandisi Ndikilo.
Aidha alitoa wito kwa kila Halmashauri kuhakikisha wanafunzi wote waliopangiwa kidato cha kwanza wamepata nafasi ifikapo mwezi june 2020.
Katika hatua nyingine Mhandisi Ndikilo alitoa agizo kwa Wakurugenzi kuhakikisha vituo vya afya vilivyojengwa kwenye maeneo yao vinaanza kufanya kazi.
Katika kikao hicho Ndikilo aliwataka watumishi kufuata maadili ikiwa ni pamoja na kusoma alama za nyakati kwa kufuata kile kinachotakiwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.