Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo Leo Juni 5 2020 amefikia uamuzi wa Kumtaka Katibu Tawala Mkoa wa Pwani kumpangia kituo kipya cha kazi Bw Jonas Nambua Afisa Misitu Halmshauri ya Rufiji.
Ndikilo ametoa uamuzi huo wakati akihutubia Mkutano wa Baraza Maalum la Madiwani Halmashauri ya Rufiji cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mwaka 2018/2019
“Nimepokea malalamiko mengi kuhusiana na Afisa Misitu wa Wilaya Rufiji nakuagiza RAS huyu abadilishiwe kituo aje mwingine hapa tuone hali itakuaje" alisema Ndikilo.
Katika hatua nyingine Mhe. Ndikilo amemtaka Katibu Tawala Mkoa kuwasiliana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhusu changamoto ya ukosefu wa Vitendea kazi Magari, vifaa vya Ofisini na Watumishi, katika Halmshauri hiyo.
"Naomba kwa kweli tuiangalie Halmashauri hii hawana vitendea kazi vya kutosha, Halmshauri hii ya Rufiji ndiyo iliyozaa Kibiti haitakiwi kusahaulika".
Ndikilo amelimbia Baraza hilo la Madiwani kuwa katika ziara yake aliyoifanya Machi 16 2020 kuangalia athari za Mafuriko Wilayani Rufiji Kijiji cha Muhoro nilitoa maelekezo ya Kuhamishwa kwa Wananchi wale kwenda kwenye eneo jipya linalomilikiwa na TFS Wakala wa Huduma za Misitu napenda kuwapa taarifa kuwa Mkuu ea Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rufiji wamekutana na Wataalam wa wakala wa Huduma za Misitu na sasa TFS wanakamilisha eneo ambalo Kijiji kitahamia Ndani ya kipindi kifupi Wananchi watahamia alisema Ndikilo.
Aidha amehimza Halmshauri hiyo kuanza kufikiria Miradi mipya ya Kimkakati itakayowasaidia kuongeza Mapato. vilevile amewataka kufunga hoja zote zilizobaki ndani ya siku 14.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.