Wilaya ya Rujiji imepata tiba ya changamoto mgogoro wa ardhi kati ya wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Nyamwage kwa kuligawia kila kundi eneo la kuendeshea shughuli zake.
Katika kutekeleza hilo, Serikali ya Wilaya hiyo imetumia mbinu ya kugawa vitalu vya ufugaji upande mmoja na vya kilimo upande mwingine kisha kuweka mpaka wa Mkuza wenye urefu wa Kilomita 8 na upana wa mita 30 unaoyatenganisha maeneo hayo.
Katika taarifa yake aliyoitoa wakati akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Pili Mnyema aliyafanya ziara ya kikazi wilayani humo mwanzoni mwa wiki, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mhe. Luteni Kanali Fredrick Komba alisema hali hiyo itarahisisha kubaini kundi litakalovunja utaratibu huo na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha alisema kwa sasa tayari zoezi la ugawaji wa vitalu limeanza na mpaka kufikia tarehe 30 Oktoba, 2025 wakulima na wafugaji waliopo katika eneo hilo watakuwa tayari wamekaa katika maeneo yao rasmi.
Kwa upande wake Daktari wa Mifugo Mkoa wa Pwani Ramadhani Mwaiganju alisema wakulima 668 tayari wamepatiwa vitalu vyenye wastani wa ekari 3 kila mmoja na wafugaji 53 wamepatiwa wastani wa ekari 100.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.