Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa( 2023) ,Abdallah Shaib amehimiza wananchi kuongeza matumizi ya Nishati Mbadala (gesi) na kutunza Mazingira.
Rai hiyo ameitoa leo Mei 16 ,katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Bagamoyo,wakati akipokea taarifa na kukagua shughuli za mabadiliko ya tabia nchi, hifadhi ya Mazingira na Utunzaji wa Vyanzo vya maji -upandaji wa miti, Shule ya Sekondari Hassanal Damji, pamoja na kugawa mitungi ya gesi kwa baadhi ya mama lishe kata ya Magomeni Wilayani humo.
Aidha amezisisitiza, Sekretariet za Mikoa na Halmashauri za wilaya, kusimamia sheria,kanuni na miongozo inayotolewa na Serikali kuhusu uhifadhi wa Mazingira,misitu na raslimali zake, Vyanzo vya maji na maeneo tengefu.
Shaib amezitaka pia kusimamia sheria ndogo ndogo zinazotungwa na Halmashauri hizo kwa lengo la kuhifadhi Mazingira,usafi na vyanzo vya maji.
Vilevile, Shaib ameitaka jamii kuepuka matumizi ya taka ngumu,vifungashio vya plastic ambavyo kwa kiasi kikubwa vinaharibu Mazingira.
Pia ufugaji kwa kukusanya makundi makubwa ya mifugo pamoja na uchimbaji madini holela pamoja na kuzuia uvuvi haramu.
Mwenge wa Uhuru ulipokelewa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ukitokea Halmashauri ya Chalinze,ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Shauri Selenda alieleza, Mwenge huo utapitia miradi Tisa yenye thamani ya sh.Bilioni 2.3.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.