Katibu tawala wa Mkoa wa Pwani Rashid Mchata amefungua kikao kazi kwa wadau Asasi zinazofanya shughuli zinazohusiana na masuala ya Wanawake kutoka Halmashauri za Kibaha Mjini, Kisarawe na Chalinze unaoendeshwa na Shirika la Un Women.
Kikao hicho ambacho kimeandaliwa na Shirika la Un Women kimefanyika katika Halmashauri ya Chalinze kimelenga kujadili namna ya kuhamasisha ushiriki wa Wanawake kwenye masuala ya uongozi katika chaguzi zijazo.
Akifungua kikao hicho Mchata amesema Serikali ipo kuhakikisha Wanawake wanashiriki katika vyombo mbalimbali vya maamuzi
Amepongeza Un Women kwa namna inavyoshirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi yake huku akisema Mkoa huo unasimamia Wanawake kushiriki katika mambo mablimbali ya uongozi.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Pwani Grace Tete alisema katika hatua za kuandaa bajeti ya Mkoa huo Serikali imeendelea kuzingatia masuala ya kijinsia katika bajeti zake.
Tete pia alisema wanaendelea kufuatilia majukwaa ya Uwezeshaji yaliyoanzishwa kama yanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia malengo, na kwamba mazingira wezeshi kwa Wanawake na watoto wa kike yameendelea kuwekwa Ili kuwainua kiuchumi.
Mratibu wa mradi huo unaohusiana na masuala ya uongozi kwa Wanawake Deogratias Mamiro amesema utekelezaji wa mradi huo ni katika Mikoa sita na Halmashauri 18 hapa nchini na unalenga kuleta matokeo ya kitaifa na kimataifa kwenye masuala ya Wanawake na uongozi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.