Serikali imeahidi kuzipatia fidia halmashauri zote za mkoa wa Pwani ambazo zinatoa malighafi yake kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa SGR unaondelea.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge octoba 12, 2023 wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika ukumbi wa mkoa huo ambacho kimewahusisha wakuu wote wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri, wakurugenzi wa halmshauri, wataalam na wakuu wa Idara.
Amesema kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye aliziahidi halmshauri zote kupata fedha kutokana na kutoa malighafi zinazotumika katika ujenzi wa reli ya kisasa.
Malighafi hizo zinatoka katika halmashauri kama vile Chalinze na Rufiji na kwamba viongozi wa maeneo husika watajulishwa ni lini fedha hizo watazipata.
“Pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini pia tunaishukuru kwa sababu kwa mkoa wetu tumepata bahati, hivi karibuni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametuahidi kutupa fidia ya fedha kwa sababu ya kutoa malighafi ambazo zinaendelea kutumika kwenye ujenzi wa reli ya kisasa,” amesema Kunenge.
Sambamba na hilo, pia amemtaka Meneja wa Wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA kuhakikisha ujenzi wa miradi yote ya barabara inakamilika kwa wakati ili kuwasaidia wananchi msimu wa mvua
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.