Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi Dkt .Moses Kusiluka ameeleza, Serikali inaendelea kuunga mkono juhudi za wawekezaji nchini kwa kuwekea mazingira wezeshi ili kutekeleza majukum yao kirahisi.
Vilevile ,Kusiluka amewaasa watendaji wa Wilaya na Mikoa kujenga tabia ya kukutana na wawekezaji ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi.
Hayo aliyasema leo Januari 5 katika ziara yake ya kutembelea viwanda viwili vya nguo na vipodozi vilivyojengwa ndani ya Kongani ya SINO TAN ,Kwala wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani, huku akiwa ameambatana na Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba ,Waziri wa Viwanda na Biashara na makatibu wakuu wa wizara ya Uchukuzi,Fedha,Viwanda na Biashara na Taasisi wezeshi.
Alieleza Serikali ya awamu ya sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuvutia wawekezaji, na Tanzania ni eneo salama kwa uwekezaji.
"Kwa muda mfupi tumeona matokeo ya malengo yenu, na tunaendelea kuwapa uhakika kuwa tunalipa umuhimu wa juu sana kongani hii" alieleza Kusiluka.
Awali mratibu wa mradi wa kongani ya Sinotan Jensen Hung alisema, kongani ya Sinotan ,wanatarajia kujenga viwanda vya kati na vikubwa 300 na kutoa ajira za moja kwa moja 100,000.
Waziri wa viwanda na Biashara,Dkt. Ashatu Kijaji alieleza, kama wizara wanatamani kuona kongani hiyo inajaa viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge alieleza viwanda vingi vinasuasua kutokana na upungufu wa nishati ya umeme na gesi.
Hata hivyo, mkoa umejipanga vizuri katika suala la uwekezaji na ujenzi wa viwanda.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.