Serikali imesitisha mara moja shughuli zilizokuwa zinafanywa na wananchi katika eneo la mto Maleta Wilaya ya Mafia mkoani Pwani kwa kuwa ni chanzo pekee cha maji katika visiwa hivyo na ni eneo la uhifadhi na mazalia ya viumbe wa baharini.
Tamko la kusitishwa kwa shughuli za Kibinadamu katika eneo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati wa mkutano wa hadhara alioufanya katika kisiwa kidogo cha Chole kilichopo wilayani Mafia kuzungumzia maamuzi ya baraza la Mawaziri kufuatia taarifa ya timu ya mawaziri nane wa kisekta ambao walifika na kutafuta suluhisho la migogoro ya ardhi iliyokuwepo Mkoani humo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Chole Ally Mgeni amepongeza uamuzi wa serikali wa kusitisha shughuli za kibinadamu katika mto huo.
Katika maamuzi hayo, Kunenge amemuelekeza Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mafia kuhakikisha mwekezaji katika kisiwa kidogo cha Chole aliyesajiliwa kwa jina la "Chole Conservation Company" haruhusiwi tena kuhuisha mkataba wake wa uwekezaji katika kisiwa hicho kwani eneo alilowekeza alilipata kwa udanganyifu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.