Serikali imewasihi wawekezaji mbalimbali kuwekeza kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani ili kuweka kuinua sekta ya uwekezaji na utalii sanjali na kupandisha pato la kisiwa hicho.
Akifunga kongamano la utalii na uwekezaji Mafia, Mkoani Pwani Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ,Agnes Kisaka Meena alieleza Mafia ni kivutio cha uwekezaji wa uchumi wa bluu na mazalia ya samaki Duniani hivyo Serikali itaendelea kutangaza vivutio vilivyopo ili iweze kujitangaza zaidi ulimwenguni.
"Tunaendelea kuinadi Mafia,ili kuvutia wawekezaji na kuongeza watalii nchini na hili limetiwa nguvu kubwa na filamu ya royal tour iliyoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan"na imani yetu wawekezaji mbalimbali na watalii wataendelea kuongezeka"
Vilevile amepongeza wilaya kwa kuandaa kongamano hilo ,ambalo limefanikiwa kwa asilimia 100.
Akitoa sifa kwa wawekezaji wa ndani amempongeza mwekezaji mkubwa Mafia Kassam ambae amethubutu kujenga mahoteli ya kutosha.
Awali mkuu wa wilaya ya Mafia Zephania Sumaye alieleza , asilimia 70 ya mapato halmashauri ya Mafia inategemea utalii na uchumi wa bluu.
Alieleza, Mafia ni kivutio cha uwekezaji katika uchumi wa bluu, ikiwemo uvuvi endelevu, ufugaji wa viumbe maji, viumbe bahari,utalii na usafirishaji baharini.
Zephania alieleza,wanaendelea kuboresha miundombinu ya uwekezaji katika miundombinu mbalimbali, kuitangaza Mafia ambapo wamejipanga kutenga maeneo na kongani ili kuvutia wawekezaji.
SERIKALI imewasihi wawekezaji mbalimbali kuwekeza kisiwa cha Mafia , Mkoani Pwani ili kuweka kuinua sekta ya uwekezaji na utalii sanjali na kupandisha pato la kisiwa hicho.
Akifunga kongamano la utalii na uwekezaji Mafia, Mkoani Pwani Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ,Agnes Kisaka Meena alieleza Mafia ni kivutio cha uwekezaji wa uchumi wa bluu na mazalia ya samaki Duniani hivyo Serikali itaendelea kutangaza vivutio vilivyopo ili iweze kujitangaza zaidi ulimwenguni.
"Tunaendelea kuinadi Mafia,ili kuvutia wawekezaji na kuongeza watalii nchini na hili limetiwa nguvu kubwa na filamu ya royal tour iliyoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan"na imani yetu wawekezaji mbalimbali na watalii wataendelea kuongezeka"
Vilevile amepongeza wilaya kwa kuandaa kongamano hilo ,ambalo limefanikiwa kwa asilimia 100.
Akitoa sifa kwa wawekezaji wa ndani amempongeza mwekezaji mkubwa Mafia Kassam ambae amethubutu kujenga mahoteli ya kutosha.
Awali mkuu wa wilaya ya Mafia Zephania Sumaye alieleza , asilimia 70 ya mapato halmashauri ya Mafia inategemea utalii na uchumi wa bluu.
Alieleza, Mafia ni kivutio cha uwekezaji katika uchumi wa bluu, ikiwemo uvuvi endelevu, ufugaji wa viumbe maji, viumbe bahari,utalii na usafirishaji baharini.
Zephania alieleza,wanaendelea kuboresha miundombinu ya uwekezaji katika miundombinu mbalimbali, kuitangaza Mafia ambapo wamejipanga kutenga maeneo na kongani ili kuvutia wawekezaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.