Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amewaelekeza viongozi wa Vijiji kuzingatia Sheria namba 5 ya ardhi katika ugawaji wa maeneo Ili kupunguza migogoro ya mara kwa mara.
Silaa ameyasema hayo Julai 2 alipofanya ziara katika Halmashauri ya Chalinze na Kibaha kutembelea maeneo yenye migogoro na kuzungumza na wananchi.
Katika Kijiji cha Chamakweza Halmashauri ya Chalinze wananchi walilalamikia kuwepo kwa mgogoro wa zaidi ya miaka 20 kati ya wakulima na wafugaji ambao imesababisha kila upande kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Sambamba na hayo pia walimueleza Waziri huyo uwepo wa uuzaji wa maeneo kiholela bila kushirikisha wananchi jambo ambalo limekuwa chanzo maelewano hafifu kati ya pande hizo mbili.
Kutokana na hali hiyo Waziri Silaa wanaonunua ardhi kufuata taratibu kwa kushirikisha wataalamui wa ardhi ngazi ya Halmashauri husika.
Ameahidi kuunda time kwa ajili ya kuhakikisha mipaka na kufuatilia uhalali wa wananchi waliohamishwa kwenye baadhi ya Vijiji katika oparesheni iliyofanyika 1974.
Mbali ya kuunda timu Waziri huyo amesitisha uendelezaji wa eneo katia Kijiji cha Kikongo ambalo wananchi 214 wana mgogoro wa muda mrefu kati yao na Mwekezaji wa Kampuni ya Trans Continental.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza katika nyakati tofauti kwenye mikutano hiyo amesema yeyote atakayebainika kuvunja Sheria hatua zitachukuliwa dhidi yake.
Pia Mkuu huyo wa Mkoa amesitisha uuzaji wa maeneo katika Kijiji cha Chamakweza kupisha timu inayoundwa na Waziri Silaa itakayofanya kazi kwenye maeneo ya mgogoro kijijini hapo.
Waziri Silaa amekutana na wananchi wa Kijiji Cha Chamakweza na Pingo katika kitongoji cha Mbala pamoja na wananchi wa Kikongo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Migogoro iliyowasilishwa kwa Waziri huyo ni pamoja na muongiloano wa wananchi Jamii ya wakulima na wafugaji na pia uwepo wa wananchi walionunua ardhi bila kufuata Sheria na taratibu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.