Mkuu wa Mkoa wa Mhandisi Evarist Ndikilo amekabidhiwa Miradi ya Sekta ya Elimu na Afya yenye thamani ya Shilingi za kitanzania milioni 425.7 ambapo miradi hiyo hiyo imetekelezwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA ) kwa kuchangia wastani wa asilimia 70 na Mchango wa Wananchi wa Vijiji vya Mkange na Saadani asilimia 30,
Miradi aliyokabidhiwa ni pamoja na Zahanati, Nyumba ya Mwalimu, Nyumba ya Mganga, Chomea taka, Matanki ya Maji, Choo, na Samani kwa ajili ya Zahanati.
Mhe Ndikilo amewapongeza Wananchi wa Kata ya Makange kwa kushirikiana na TANAPA Kupitia Idara ya Ujirani Mwema kufanikisha miradi hii mizuri ambayo ni chachu ya maendeleo ya kuboresha huduma ya Afya, Elimu na Maji Kata ya Mkange na Taifa kwa ujumla.
Ndikilo ametoa wito kwa Wananchi hao kuilinda hifadhi ya Saadani kwa kuwa miradi hiyo ni matunda ya hifadhi. Aidha, amesisitiza wananchi kuitunza miradi hiyo.
Katika Hatua nyingine Ndikilo amemuagiza Mkurugenzi wa Chalinze kupeleka mganga katika Zahanati hiyo na kuhakikisha inaanza kufanya kazi ndani ya siku 7.
Pia ameitaka Halmashaur hiyo kuwa na mawazo mapana ya kufanya zahanati hiyo kuwa Kituo cha Afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.