Kiasi cha sh. Bilioni 15 kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo iliyo chini ya Wakala wa Barabara nchini -TANROADS katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Baraka Mwambage ameeleza hayo wakati akitoa taarifa kwenye kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika mjini Kibaha, kikihusisha viongozi wa serikali na watendaji kutoka ngazi za wilaya, mkoa, TANROADS na TARURA.
Amesema hadi kufikia robo ya mwaka wa fedha 2023/2024 sh. Milioni 18.3 zimepokelewa katika mkoa huo kuendelea na shughuli mbalimbali za miradi ya barabara.
Meneja huyo amebainisha kwamba, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 na 2022/2023 bajeti ya mkoa imeongezeka sh. Bilini 10.811 katika fedha za miradi ya maendeleo.
Mhandisi Mwambage ameeleza vikwazo wanavyokutana navyo kuwa ni pamoja na wizi, uharibifu wa thamani za barabara na uvamizi wa hifadhi.
Pia ameeleza kuwepo kwa malalamiko kutokana na ucheleweshaji wa malipo ya fidia sehemu zilizofanyiwa tathmini.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amezitaka TANROADS na TARURA kutengeneza barabara kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji muhimu ili kuondoa vikwazo vya kutopitika muda wote.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.