Mkoa wa Pwani ,umefanya mnada wa kwanza wa zao la kibiashara la ufuta ,na kufanikiwa kuu tani 1,231 kati ya tani 3,118 zilizokwenda sokoni kwa bei ya juu ya sh.2,172 kwa kilo moja .
Tani zilizokwenda sokoni zimenunuliwa kupitia mfumo wa sanduku (box) kwa wateja watatu waliojitokeza tofauti na matarajio ya wengi kuwa tani nyingi zingenunuliwa kupitia mfumo wa kielektronik wa TMX ambapo amejitokeza mteja mmoja kwa mkoa wa Pwani kwa bei ya sh.1,750 ukilinganisha na minada ya Dodoma na Mtwara ambayo walifanikiwa .
Akizindua mnada huo wa kwanza uliofanyika ,wilaya ya Kibiti ,mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema tani zinazotarajia kuzalishwa kwa mkoa huo kwa msimu huu ni tani 10,000 .
Alieleza ,tani 1,231 za ufuta zilizokwenda sokoni ni katika ghala kuu la Ikwiriri na Kibiti .
Hata hivyo ,mkuu huyo wa mkoa alitangaza mnada wa pili utafanyika Juni 19 ,mwaka huu .
";Mkoa wetu umetumia mifumo hii miwili, bei kubwa imetokana na mfumo wa sanduku ,kupitia mtandao bei ni ya chini na mnunuzi aliyejitokeza ni mmoja ,nawaomba TMX mjipange kutafuta soko ,maana mikoa mingine imefanikiwa ,ichunguzwe kama kuna mtu anawahujumu ijulikane achukuliwe hatua " alisisitiza Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo alitaja changamoto kubwa, iliyopo kwasasa ni kukwama kwa ufuta kwenye maghala ya vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS )na kushindwa kufikishwa kwenye maghala makuu kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu .
Alielekeza ,wanunuzi waelekezwe ufuta ulipo katika maghala hayo ,na ununuliwe ukiwa huko kwa utaratibu wa mfumo wa stakabadhi ghalani na si vinginevyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.