Vyombo vya habari vya kijamii vimehimizwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu huduma ya M-Mama na matumizi sahihi ya namba ya dharura 115, baada ya ripoti kuonyesha kwamba baadhi ya wananchi wamekuwa wakiitumia namba hiyo kwa matumizi yasiyokusudiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Kusirye Ukio, Afisa Afya wa Mkoa wa Pwani, David Vuo, alitoa wito huo tarehe 6 Novemba 2024, katika kikao kazi kilichoandaliwa na M-Mama na kuhusisha wajumbe kutoka mikoa sita ambao ni amaafisa Habari wa Mikoa.
Alieleza kuwa kikao hicho kililenga kuandaa mikakati ya jinsi vyombo vya habari vya kijamii, kwa kushirikiana na waratibu wa huduma ya M-Mama katika mikoa na wilaya, vitakavyoweza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma hiyo na matumizi sahihi ya namba 115.“Tunapomaliza kikao hiki, kila Mratibu atakuwa na jukumu la utekelezaji.
Niombe tuendelee kufanyia kazi kama tulivyokubaliana,” alisema Vuo.Huduma ya M-Mama ni huduma ya dharura inayotolewa kwa wajawazito, wanawake waliojifungua (chini ya siku 42), na watoto wachanga (chini ya siku 28) wanaohitaji msaada wa haraka wa kiafya.
Huduma hii inapatikana bure kwa kupiga namba 115 kutoka mitandao yote ya simu, na inaweza kufikiwa muda wowote na mahali popote nchini Tanzania Bara na Zanzibar.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.