Wakazi wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani wameiomba Halmashauri ya Wilaya hiyo kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi kinachojengwa na Serikali kwa lengo mahususi la kuvutia Mji wa Kisarawe, kukua kibiashara na kiuchumi.
Hayo wameyasema wakati Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo alipofanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya maendeleo Wilayani humo , na kukagua barabara ya Chole , Vikumburu pamoja na ujenzi wa kituo hicho.
Aidha Diwani wa kata ya Kisarawe Abel Mudo amesema kuwa, kukwama kwa kituo hicho kunasababisha adha kwa abiria wanaotumia kituo hicho kusafiri kwani kilichopo ni kidogo na hakina paa la kuzuia abiria kunyeshewa na mvua na pia kudumaza ukuaji wa Mji huo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Musa Gama amesema ujenzi wa kituo hicho unagharimu jumla ya shilingi milioni 219 lakini mpaka sasa mradi unasuasua kutokana na ukosefu wa fedha.
Akizungumza mara baada ya kukagua kituo hicho Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisin Evarist Ndikilo ameiagiza Halmashauri hiyo kukamilisha haraka mradi huo ili uweze kuwasaidia wananchi kama Serikali inavyokusudia.
Aidha Mhandisi Ndikilo amewapongeza wakala wa Barabara Mijini na Vijijni TARURA kwa kuweza kuunganisha mtandao wa barabara Wilayani humo.
“Napenda kuwapokeza TARURA kwa kweli kazi mmeifanya , kwani ni kipindi kifupi sana tokea muanzishwe lakini mmefanya mambo makubwa sana kwani miundo mbinu ya barabara inaridhisha na inaendanana na thamani ya Fedha kweli mnahitaji pongezi “ alisema Mhandisi Ndikilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.