Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Morogoro wamefanya ziara ya pamoja kukagua chanzo cha maji cha mto Ruvu kufuatia uwepo wa Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakari Kunenge aliyeambatana na viongozi kutoka taasisi ya Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu pamoja na DAWASA, wamefika katika eneo la kidakio cha Ruvu juu na Ruvu chini na kujionea ongezeko kubwa la maji katika mto huo.
Akizungumza na Wanahabari Mhe. Abubakari Kunenge amesema kuwa Mwaka huu ni wa neema kwa kuwa hali ya maji katika mto Ruvu na kutoa wito kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni na mito kuchukua tahadhari ili kuepukana na majanga ya mafuriko yanaoyoweza kujitokeza.
Awali Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/ Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy ametoa tathimini ya hali ya maji katika mto Ruvu ambapo mpaka sasa ongezeko la maji ni asilimia 69 kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika safu za milima ya Uluguru.
Aidha Mhandisi Mmassy amebainisha kuwa Bodi inaendelea na shughuli za uhifadhi wa vyanzo vya maji na kuhakikisha rasilimali hiyo inakuwa endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo pamoja na kujenga mabirika ya kunyweshea mifugo kupunguza uharibifu wa kingo za mito uliokuwa ukisababishwa na mifugo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.