Wananchi wa Mbuchi na mbwera Kibiti tunamshukuru Mhe Rais kwa Ujenzi wa Daraja la Mbuchi.-Kunenge.
Mhe Kunenge ameyasema hayo leo November 29, 2022 wakati wa Ziara ya Mhe Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua Ujenzi wa Daraja hilo na kusalmia Wananchi wa Mbuchi .kulikuwa na Mgogoro.
Tulikuwa na Changamoto kubwa ya Daraja hapa Mhe Rais ameleta fedha na Daraja hili linejengwa. Eneo hii ilikuwa hliipitki.
Mhe Kunenge ameeleza kuwa Eneo hili la Mbuchi ni Eneo la Kimkakati kwa Uchumi wa Mkoa kwani kina shughuli kubwa za Kilimo na Uvuvi.
Mhe Rais amefanya kazi kubwa hana ubaguzi anatuhudumia na kupeleka huduka kule kwenye Changamoto zaidi.
Wilaya ya Kibiti na Rufiji shughuli kubwa ni la Kilimo korosho, Mpunga Ufuta. "Tuna Uwekezaji Mkubwa kilimo cha Mpunga Wilaya ya Kibiti" Ameeleza Kunenge
Wawekezaji wanakimbilia eneo hili kwa sababu Lina Maji na Ardhi nzur yenye Rutuba.
Kunenge ameeleza Kutokana na Changamoto ya Mabadiliko ya Tabia Nchi Wafugaji Wengi wamehamia Wilaya ya Rufiji na Kibiti. Hali inayopelekea Mifugo kuwa mingi kuliko ukubwa wa Ardhi iliyotengwa kwa malisho.
Mhe Kunenge ameeleza Mkoa Unaendelea na kutoa elimu kwa Wakulima kufuga Mifugo kulingana na Ardhi ya Malisho. Ameeleza Mkoa unatekelezwa Mpango wa Ranchi Ndogo na wameanza kwa Wilaya ya
kisarawe tuna Ufugaji na kibiti tuna Ufugaji wa Ranchi Ndogo.
Ameeleza kuwa wametenga maeneo kibiti na Rufiji na watawapa Wafugaji ili wafuge kisasa.
"Tuwe na Ng'ombe wachache wa kisasa" Ameeleza Kunenge.
Naye Mhe Waziri Mkuu ameridhishwa na Ujenzi wa Dajara Hilo amepongeza Taasisi za TANROADS na TARURA kwa kazi nzuri ya Usimamizi na Ujenzi wa Daraja hilo.
Ameeleza Ujenzi wa Daraja hilo ni dhamira ya Serikali ya Kuhakisha inawafikia Wanchi mpaka Vijijini. Ameeleza ndiyo maana Serikali imeanzisha Wakala wa Serikali wa Barabara Vijijini TARURA. Amemwagiza Waziri TAMISEMI Kushughulikia Ujenzi wa Barabara Unganishi kutokea Mhoro kufika Mbuchi. Amewataka Wananchi kuchangamkia Fursa za Kiuchumi zilizopo Eneo hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.