Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo amemtaka kamanda wa Polisi kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo kuhakikisha kua wale wanaowapa mimba wanafunzi wanachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mhandisi Ndikilo alitoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa kilichofanyikja kwenye ukumbi wa Ofisi mkuu wa Mkoa Mjinini Kibaha na kuhudhuria na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya.
Mhandisi Ndikilo alisema kuwa , takwimu za mimba zinasikitisha huku wanaochukuliwa hatua za kisheria wakiwa wachache ukilinganisha na waliopewa mimba.
Pia alisema kuwa , ni marufuku kwa wazazi/walezi ama polisi kumaliza kesi za mimba kinyemela na badala yake wahusika wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe funzo kwa wengine na kukomesha tabia hiyo.
“Hakuna kesi ya mimba inayomalizwa na wazazi au walezi kwa kufanya vikao vyao wenyewe , wahusika wapatikane na jeshi la polisi liwafikishe mahamakani watuhumiwa na sheria ichukue mkondo waka” alisema Mhandisi Ndikilo.
Akiwasilisha taarifa ya Elimu , Afisa elimu wa mkoa wa Pwani Abdul Mauld alisema kuwa wanafunzi waliopata mimba na kuacha shule kuanzia January hadi Disemba 2018 katika shule za misingi na sekondari ni 235.
Maulid alisema kati ya wanafunzi ha 80 ni kutoka shule za msingi na 155 wa shule za sekondari kutoka kila Wilaya za Mkoa huo.
Aidha alieleza katika kikao hicho kuwa Hamashauri ya Chalinze wanafunzi 17 wa shule za msingi na 29 wa sekondari walipata mimba, katika Wilaya ya Mkuranga ni wanafunzi 20 wa shule za msingi na 28 Sekondari.
Wilaya nyingine ni kisarawe wanafunzi 12 wa msingi na sekondari 21 , Rufiji wanafunzi 14 na 17 wa sekondari , katika wilaya ya kibiti waliopata mimba wa shule za msingi ni 8 na sekondari 28.
Pia aliainisha idadi ya wanafunzi waliokuwa na mimba kutoka mafia kuwa ni 8 wa sekondari na Wilaya ya Bagamoyo 6 wa shule zamsingi na 4 wa sekondari Halmashauri ya Mji Kibaha wanafunzi wawili wa msingi na 15 Sekondari na Halmashauri ya Wilaya Kibaha mmoja wa msingi na 5 wa Sekondari.
Suala hili lilileta taharuki kwa wajumbe wa kikao hicho ambao kwa pamoja walidhamiria kulivalia njuga na kulipangia mkakati wa kuondoana tatizo la mimba mashuleni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.