Watumisha wa umma mkoani Pwani wameaswa kutumia mfumo wa kidijitali wa manunuzi ya umma (Nest) ambao unasimamiwa na mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya Umma (PPRA).
Rai hiyo imetolewa leo Juni 4, 2024 Rai na Kaimu Katibu Tawala Mkoa huo Shangwe Twamala wakati akifungua kikao kazi juu ya matumizi ya mfumo huo.
Twamala ameeleza kuwa matumizi ya mfumo huo ni maagizo ya Serikali hivyo manunuzi yote katika ofisi za Umma lazima yatumie mfumo huo.
"Ni kosa kubwa kufanya manunuzi bila kutumia mfumo wa NeST na endapo mtumishi wa umma atafanya manunuzi nje ya mfumo atachukuliwa hatua kali pamoja na kutozwa faini," amesema Twamala.
Ameeleza kuwa mfumo huo ni rahisi na rafiki kuutumia. Pia umesaidia kuondoa tabia za urasimu iliyokuwa ikijitokeza kipindi cha mfumo wa Zamani pia umeongeza ushilikishwaji wa watumiaji kwa kuwa wanaomba mahitaji kwa kutumia mfumo.
Pia amewataka makatibu tawala wa Wilaya zote mkoani humo kuzisimamia halmashauri vizuri na kuhakikisha kuwa zinafanya manunuzi yote kwa kutumia Mfumo huo wa NeST.
Kikao kazi hicho cha siku moja kimewahusisha Wakuu wa Sehemu na vitengo na wasidizi wao, Makatibu Tawala wa Wilaya na wahasibu wa Wilaya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.