Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarisrt Ndsikilo amewataka wawekezaji Mkoani humo kuzingatia athari za uchafuzi wa Mazingira kabla ya kuanzisha Viwanda. “Uanzishwaji wa Viwanda katika Mkoa wa Pwani lazima uendane pia na masuala ya Mazingira. Tathimini ya Athari ya Mazingira ni muhimu” Ameyasema hayo Februari 16,2021 wakati wa ziara ya Mhe. Ummy Mwalimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Wilayani Kibaha.
Ndikilo Amewataka pia Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC kutoa kwa wakati vyeti vya athari za mazingira ili wawekezaji wasikwame katika uwekezaji “Viwanda vingine vinashindwa kuanzishwa kwa wakati kwa kukosa cheti cha Tathimini ya Mazingira EIA Certificate’ tufanye haraka ili tusikwamishe wawekezaji ambao wapo tayari kutuletea ajira”
Amezungumzia pia uthibiti wa Taka kutoka kwenye Viwanda, Ni kweli tumetenga maeneo ya Viwanda, lakini viwanda vingine vipo kwenye maeneo ya watu. Ametaka Wizara kuangalia namna nzuri ya kutatua changamoto hii kwa viwanda ambavyo tayari vimejengwa kwenye maeneo ya watu kuliko kufunga viwanda hivyo jambo ambalo ni hasara kubwa kwa wawekezaji.
Amesema Mkoa huo unakabiliana na changamoto uchimbaji holela wa mchanga na ukataji wa misitu ovyo. Wanachimba mchanga kwenye maeneo yetu vijijini mwishoe wanaondoka na kuachia vijiji mashimo na mabwawa.“Mhe Waziri hawa waliopewa vibali vya kuchimba mchanga Pwani wadhibitiwe na sheria ili wasiache mahandaki kwenye maeneo hayo” alisitiza Ndikilo. Ameeleza pia suala la ulinzi wa vyanzo vya maji bado ni changamoto sheria ipo Mita 60 kutoka katika mto lakini Maeneo ya Mto Ruvu na Wami bado yamevamiwa.amewataka wanachi waachane na tabia hiyo na kufuata sheria inavyotaka.
Ametaja pia hatua iliyopigwa na Halmashauri za Mkoa katika kudhibiti taka ngumu, tumejitahidi lakini bado wasafiri wa mabasi wanatupa taka ngumu hovyo.” Tushirikiane na wizara kuazisha vikundi na kutoza adhabu ndogo ndogo ili kudhibiti tabia hii. Ndikilo Ameethibitisha kuwa Agizo Makamu wa Rais la kufanya Usafi la kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi linatekelezwa vizuri kwa wananchi kushiriki ipasavyo kwenye maeneo yao.
Mhe Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Ummy Mwalimu ameupongeza Mkoa huo kwa utendaji kazi na kumhakishia Mkuu wa Mkoa kuwa NEMC itaondoa changamoto ya ucheleweshaji wa vibali tathmini ya mazingira na kuacha mara moja tabia ya kuwakamata na kuwatoza faini ovyo wawekezaji
“Nilishawaambia NEMC msifanye kazi ya polisi ya kufunga kiwanda na kutoza faini. Mkiona kiwanda kinachangamoto nendeni mkakae na mmiliki wa na muone namna ya kuzitatua”alisema Mhe Ummy.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.