Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imebadilisha hali ya Kiuchumi na Kijamii katika Wilaya ya Mafia. akizungumza kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani Wilayani Mafia Juni 9 2020 cha kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG za Mwaka 21/19.
Ndikilo ameeleza Mafanikio hayo kuwa ni pamoja na Mradi wa Maji Jibondo.
Jibondo ni Miongoni mwa Kisiwa kidogo katika Wilaya ya Mafia.
“Tangu kuanzishwa kwa Kijiji hiki hapakuwa na maji ya uhakika. kukamilika kwa mradi huu Wanachi zaidi 2000 wamepata Maji safi na salama, wameodokana na uwezekano wa kupata magonjwa yanayosababishwa kwa kukosa maji safi na salama na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata maji" alisema Ndikilo.
Ametaja pia Ujenzi wa Meli itakayokuwa ikifanya safari zake kati ya Nyamisati na Mafia ambayo ni ahadi ya Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa umefikia asilimia 70 na inategemewa kukamilika ifikapo tarehe: 30 Juni 2020
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa amekubaliana na Ombi la Baraza la Madiwani Mafia kuwa Meli hiyo ipewe jina la "MV Papa Potwe".
“Nimelichukua jina hilo tutawasiliana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ili Meli hii ipewe jina hilo” alisema Ndikilo.
Alifafanua kuwa Papa Potwe (Whale sharks) ni aina ya samaki anayepatikana kisiwani mafia na Watalii wengi hufika kisiwani hapo kumtazama.
Aliendelea kusema Meli hiyo ya Serikali inajengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 5.3 na itakuwa na Uwezo wa Kubeba Abiria 200, Tani 100 za mizigo na Magari 6 .
Amempongeza Mwekezaji Binafsi ambaye hivi karibuni ameanza kutoa huduma ya Usafiri wa Meli kati ya Nyamisati na Mafia."Namshukuru Waziri mwenye dhamana kutoa kibali kwa Meli hii alisema Ndikilo.
Meli ya MV Captain 1 imeanza safari zake tarehe 11 Mei, 2020 ina uwezo wa kubeba abiria 180 na Mizigo Tan 100.
Ndikilo ametoa maelekezo kwa Meneja TANROAD Mkoa kuanza Ujenzi wa Barabara ya Bungu -Nyamisati yenye urefu wa kilometa 40.1 kwa kiwango cha changarawe. ameeleza kuwa Barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa itarahisisha usafiri wa Mizigo na Abiria kutoka na kuingia Bandarini hapo.
Aidha ametoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu LATRA Mkoa wa Pwani kuanzisha njia hii ya Magari ya kusafirisha Abiria kutoka Dar es salaam kwenda Nyamisati na kutoa leseni ya usafirishaji kwa wadau wa usafiri kusafirisha abiria. kwa kufanya hivo kutakuwa na usafiri wa uhakika unaotabirika alisema Ndikilo.
kuhusu zao la Korosho Mhandisi Ndikilo ameeleza kuwa ndani ya miaka mitatu zao la Korosho limefanya vizuri akitoa takwimu za uzalishaji amesema uzalishaji umeongezeka kila mwaka, kwani kwa mwaka 2016/17 walizalisha Tani 8, 2017/18 Tani 104.
Katika hatua nyingine Ndikilo ametaka suala la Mamlaka ya Hifadhi ya Bahari Mafia kumiliki maeneo makubwa kurekebishwa. "Mamlaka hii inahodhi maeneo makubwa mpaka ya wavuvi, Halmshauri hii haina maeneo haikusanyi mapato ipasavyo" Mgongano huu wa kisheria tulishafikisha kwa Mawaziri wenye dhamana iliurekebishwe alisema Ndikilo.
Ndikilo pia ameitaka Halmshauri ya Mafia kubuni Miradi mipya ya Kimkakati itakayoombewa fedha Wizara ya Fedha, ametaja Mradi uliobuniwa wa Mafia Tourist City upimaji wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za kitalii kuwa ni mradi Mzuri wenye tija kama utapewa fedha na Serikali utanufaisha sana Halmshauri hiyo,
katika Kikao hicho Ndikilo amewaondoa Maafisa Uvuvi wawili kwenye Halmshauri hiyo kwa utendaji wao mbovu na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato yatokanayo na Uvuvi. amemuelekeza Katibu Tawala Mkoa kuwapangia Vituo vipya Maafisa hao Bw. Ayubu Sobu na Alfred Boa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.