Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametoa wito kwa Wazazi wa watoto kuwa karibu nao wakifuatilia maendeleo yao sambamba na kuwakagua badala ya kuacha wajibu huo kufanywa na wasaidizi wa kazi za nyumbani.
Kunenge ameyasema hayo wakati akizindua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto kwa mkoa wa Pwani uliyofanyika leo Oktoba 3, 2023.
Amesema wapo wazazi na walezi ambao wamejikita zaidi kupambana na shughuli za kuwaingizia kipato na kuacha suala la malezi kufanywa na wadada wa kazi jambo ambalo linakinzana na malezi.
"Mbali ya kusimamia wazazi na walezi pia mnatakiwa kuwakagua watoto wenu mara kwa mara na kutenga muda wa kuzungumza nao," amesema.
Katika hatua nyingine, Kunenge ameziagiza Halmashauri za mkoa huo kutenga bajeti kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Programu hiyo pamoja na kutoa elimu kwa jamii ya kuwaweka watoto salama.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.