Sunday 22nd, December 2024
@Kuanzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa -TAMCO-Barabara ya Zamani-Viwanja vya Staendi ya Zamani Mailimoja Kibaha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani imeandaa mbio za Polepole (Jogging) maalum kwa ajili ya uhamasishaji Wananchi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
‘Jogging’ hii imepangwa kufanyika tarehe 12 Oktoba, 2024 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 4.30 asubuhi na itaanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuhitimishwa katika viwanja vya Stendi ya Zamani Mailimoja Mjini Kibaha. Mkuu wa Mkoa, Mhe. Abubakar Kunenge anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika shughuli hiyo.
LENGO
Lengo la mbio hizo ni kuhamasisha ushiriki wa Wananchi katika kujiandikisha, kugombea nafasi mbalimbali na kuchagua viongozi kwa kupiga kura.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.