Wednesday 4th, December 2024
@OFISI YA MKUU WA MKOA WA PWANI
TANGAZO
KATIBU TAWALA MKOA WA PWANI ANAPENDA KUWAKUMBUSHA WANANCHI WOTE WANAOKUJA KUPATA HUDUMA KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA PWANI KUWA HUDUMA ZOTE ZINATOLEWA BURE BILA MALIPO YEYOTE.
HUDUMA HIZO ZITATOLEWA KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI MPAKA SAA 9:30 ALASIRI.
HIVYO WANANCHI WOTE MNATAARIFAIWA KUWA HUDUMA ZOTE ZA SERIKALI NI BURE. NA KAMA ITATOKEA KUNA MALIPO BASI MALIPO HAYO YATAFANYIKA KWA KUPEWA KUMBUKUMBU NAMBA (CONTROL NUMBER) NA SI VINGINEVYO.
KATIBU TAWALA ANAWATADHARISHA WANANCHI WASIKUBALI KUFANYA MALIPO YA AINA YEYOTE YALE KWA KUTUMA FEDHA KWENYE SIMU KWANI WATAKUWA WAMETAPELIWA.
PIA ANAWATAHADHARISHA WANANCHI WOTE ENDAPO WATADAIWA FEDHA KWA AJILI YA KUPATIWA HUDUMA BASI WATOE TAARIFA MARA MOJA KWENYE OFISI ZA UTAWALA ZILIZOPO KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA
MWISHO KABISA ANAWAKUMBUSHA KUWA HUDUMA ZOTE ZA SERIKALI NDANI YA OFISI YA MKUU WA MKOA NI BURE NA HAKUNA MALIPO YA AINA YEYOTE ILE
ASANTE SANA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.