UTARATIBU WA KUTOA LESENI YA BIASHARA.
Ili Mfanyabiashara aweze kupata Leseni ya Biashara, lazima aombe kwa Mamlaka husika:-
Wizara ya Viwanda na Biashara kwa leseni za kundi “A” na Halmashauri kwa leseni za kundi B. Fomu ya maombi ya leseni za Biashara TFN Na. 211 ya 2004 imeonesha vizuri makundi haya. Mfanyabiashara anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:-
i. Kujaza fomu ya maombi ya Leseni za Biashara (fomu inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (www.pwani.go.tz) au fika ofisi za Biashara za Halmashauri za Wilaya za Bagamoyo, Kibaha Wilaya , Kibaha Mji, Kisarawe, Mkuranga, Mafia, Rufiji, Chalinze na Kibiti.
ii. Ambatanisha nyaraka kama inavyojieleza katika fomu ya maombi (TFN 211 ya 2004) na kuwasilisha Wizarani/ Halmashauri kwa ajili ya ukaguzi (assessment) na kujulishwa kiasi cha ada cha kulipia;
iii. Kwa Biashara za A, fanya malipo kwenye Benki utakayoelekezwa na Wizara ya Viwanda na Biashara
iv. Kwa Biashara za kundi B fanya malipo kwenye Benki utakayoelekezwa na Halmashauri husika;
v. Wasilisha “pay in slip’ ya Benki na kufuata maelekezo mengine utakayopewa na Mamlaka ya leseni husika,ili kupata risiti halali ya Serikali;
Mkoa unawashauri Wananchi wote na hasa wafanyabiashara kuwa hakuna urasimu wowote wa upatikanaji wa leseni za Biashara.Leseni za Biashara hutolewa kwa muda wa siku moja, endapo nyaraka zote zimekamilishwa na mwombaji.
Mwombaji anatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo zikiambatanishwa na Ombi Lake:
a. Nakala ya kuandikisha hati ya jina la Biashara au kampuni (photocopy of certificate of incorporation & Extract);
b. “Memorandum, and Articles of Association” ambazo zitaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kisheria kufanya biashara inayoombwa, pamoja na majina ya wamiliki wa kampuni, hisa zao na utaifa wao.
c. Uthibitisho wa uraia kwa kuwasilisha, nakala ya hati ya kusafiria nje ya Nchi ya Tanzania au hati ya kusafiria katika nchi za Afrika Mashariki, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo(Affidavit) kuonyesha kuwa ni Mtanzania, na kama mgeni ataleta hati ya kuishi nchini daraja la kwanza (Residence permit class A);
d. Endapo wenye hisa wote wapo nje ya Nchi itabidi maombi yaambatane na hati ya kiwakili (Power of Attorney) ya kumpa Mamlaka raia wa Tanzania, raia wa kigeni mwenye hati ya kuishi nchini daraja “A” au hati ya kufanya kazi nchini daraja “B” inazoainisha kuwa anasimamia kampuni husika.
e. Nakala ya usha hidi wa maandishi kuwa ana mahali pa kufanyia biashara (lease agreement, Title deed, Certificate of Occupancy, e.t.c)
f. Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (Tax payer Identification Number – TIN).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.