Jeshi la Polisi Mkoa Pwani limewakamata wahamiaji haramu 10, kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake mwanzoni mwa wiki hii, Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani ACP Jonathan Shanna alisema, wahamiaji hao ambao ni raia wa Ethiopia walikamatwa jana Majira ya ya sa 05:30 asubuhi wakiwa wamefichwa porini katika maeneo ya Pingo shule ya msingi, tarafa ya Chalinze baada ya jeshi la Polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema .
Aidha Kamanda Shanna aliwataja wahamiaji hao kuwa ni pamoja na Tegan Alam19, Abraham Wolde19, Musama Kamal 16, abush Tamaskel 16 na Ayela.
Wengine ni Ngusie Kachine 18, Zarabal Faisa 16, Tsedilj Yshge 19, Teyey Ally 18 na Tuktigo Chemag17.
Kamanda Shanna aliendelea kusema, kuwa watuhumiwa wote hao watafikishwa katika idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.
“Juhudi za kuwatafuta watu walioshiriki katika kuwaingiza nchini wahamiaji hao haramu bila kufuata taratibu za kisheria zinaendelea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.