Mkuu wa Mkoa wa Pwani amepokea Vifaa vya Kunawia Mikono kutoka Kampuni ya Motisun Group vyenye thamani ya Shilingi 6,250,000/= ikiwa ni jitihada za Mkoa kushirikiana na Wadau katika Mapambano ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Akizungumza wakati wa upokeaji wa vifaa hivyo leo tarehe 23 April 2020 Ndikilo amesema vifaa hivi ni vitagawanywa kwenye maeneo yenye kuhudumia na kukutanisha watu wengi ikiwemo Hospitali ya Mkoa na za Wilaya, Kituo cha Matibabu ya Covid 19 Lulanzi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na Masoko.
Mhandisi Ndikilo ametumia wasaa huo kuwakumbusha Wananchi wanaotumia usafiri wa Umma(Daladala) .
" Wananchi tuvae barakoa na kuzingatia level sit kwenye vyombo vya safari hii ni kwa afya zetu hata mkisimama si kwa hasara ya mtu mwingine ni wewe na familia yako" alisema Ndikilo.
Aidha amewakumbusha wazazi kuwa Serikali imefunga Shule hivyo amewataka kuzuia watoto wao kuzurura Mitaani.
Akikabidhi Msaada huo Mwakilishi wa Kampuni ya Motisun Group Abubakar Mlawa alisema kuwa Msaada huo wanautoa maeneo mbali mbali Nchini ili kuthibiti maambukizi ya Virusi vya Corona.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.