Serikali imetoa shilingi bilioni tatu nukta nane kwa ajili ya ununuzi wa kivuko cha kisasa kwa ajili ya kusafirishia abiria kutoka bandari ya Nyamisati wilayani Kibiti kwenda Wilayani Maifa ili kuondoa tabu wanaoipata wananchi wa mafia kusafiri kwa kutumia boti ambazo zinahatarisha maisha yao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Biashara la Mkoa huo kilichofanyika Mjini Kibaha.
Baraza la biashara Mkoa wa Pwani limefanyika hii leo mjini Kibaha kujadili changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya biashara katika maeneo mbalimbali za mkoa huo pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto hizo hili kuwezesha sekta hiyo kukua na kuongeza mchango wake kwenye pato la taifa.
Mhandisi Ndikilo ndiye anayefungua kikao hicho ambapo pamoja na mambo mengine ametangaza hali ya neema kwa wakazi wa visiwa vya Mafia kwamba serikali imetoa shilingi bilioni tatu nukta nane kwa ajili ya ununuzi wa kivuko kwa ajili ya kusafirishia abiria kutoka bandari ya Nyamisati iliyoko wilaya ya Kibiti kwenda wilayani Mafia.
Aidha amesema kuwa ununuzi wa kivuko hicho utarahisisha usafiri wa kuingia na kutoka katika visiwa vya Mafia jambo ambalo litafungua visiwa hivyo kibiashara na kuvutia wawekezaji wengi kwenda kuwekeza katika visiwa hivyo na hivyo kuwataka wakala wa ufundi nchini- TEMESA wanaosimamia ununuzi huo kuharakisha mchakato wa kumtafuta mzabuni wa kujenga gati katika Bandari ya Mafia na Nyamisati ili meli hiyo itakapokamilika iweze kuanza kazi mara moja.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mafia Erick Mapunda ameliambia baraza hilo kwamba halmashaurio yake inaendelea na jituhada za kutafuta usafiri wa uhakika wa kusafirisha abiria kwenda visiwani humo ambapo hadi sasa halmashauri hiyo imefanya mazungumzo na chuo cha bahari nchini kutoa meli yake ili itumike kusafirishia abiria kwenda Mafia kuanzia Dar es Salaam
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.