Serikali imeridhia kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa eneo la kiuchumi la Bagamoyo linalojumuisha ujenzi wa bandari mpya pamoja na ukanda maalum wa viwanda.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mipango na Uwekezaji prof. Kitila Mkumbo kwenye kikao maalum cha kupokea taarifa ya upembuzi yakinifu na mpango kabambe wa ujenzi wa mradi huo kilichofanyika katika chuo cha uvuvi Mbegani, Bagamoyo.
Amesema mradi huo ambao utakaogharimu kiasi cha shilingi trilioni 11 utajengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta 9800 ambazo tayari Serikali imepima hekta 5473 kati ya hizo na kuanza kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi huo.
Ameeleza kuwa Mradi huo utajumuisha ujenzi wa ukanda maalum wa viwanda, ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo, eneo huru la biashara na huduma nyingine 19 mkoani Pwani.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge pamoja na baadhi ya wakazi wa mkoa huo wamesema wanamatumaini makubwa na mradi huo na wanaungojea kwa hamu kubwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.